Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi (Nondo)Mahakamani


Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi mbaye anaitwa Nondo, amefikishwa katika mahakama ya wilaya mkoani Iringa baada ya kutolewa jijini Dar es salam ambapo alihitajika kwa ajili ya mahojiano na viongozi wa ulinzi na usalama.

Nondo amesomewa shitaka lake ambapo anadaiwa kutoa taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii na kuzusha kuwa ametekwa.

Nondo amenyimwa dhamana na kurudishwa rumande baada ya hakimu kusoma kifungu ambacho kinamfanya asimpe dhamana Mwenyekiti huyo wa mtandao wa wanafunzi.

 RECOMMENDED FOR YOU:

Join Our New Telegram Group For Jobs, Education, Scholarships and All Updates,  CLICK HERE

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad