Ads Area

SPORTS AND GAME TO DAY: MNARA AFUNGUKA MAZITO GAME LA SIMBA...!


UBINGWA WA SIMBA: Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara amewasihi mashabiki wa Simba kufika uwanjani kesho kwa wingi wakiwa wamevalia kiubingwa.

Amewaasa mashabiki kuwa wastaarabu na kumtia moyo Rais Magufuli ambaye ndiye mgeni rasmi katika shughuli ya kukabidhi kombe katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Manara pia amewapoza mashabiki wa watani wao wa jadi, Timu ya Yanga kutojisikia vibaya kwa wao kuwa wakwanza kukabidhiwa Kombe na Rais wa nchi na kwamba wao wamekuwa waanzilishi wa vingi mara zote.

"Sisi tumekuwa wa kwanza kuchukua ubingwa, kujenga jengo kubwa na wa kwanza pia kukabidhiwa ubingwa na Rais," alijitapa Haji Manara.

Amesema soka ni mchezo wa amani na unaounganisha watu wote hivyo amewaomba watakaohudhuria kujitahidi kuwa wastaarabu na kuacha tofauti zao za kidini, itikadi na vyama na kufurahia uwepo wa shughuli hiyo.

 RECOMMENDED FOR YOU:

Join Our New Telegram Group For Jobs, Education, Scholarships and All Updates,  CLICK HERE

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad