Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 25, Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amesema lengo ni kutoa fursa kwa wananchi ambao hawakuweza kuahiliwa katika awamu tatu kupata nafasi hiyo.
Amesema tume imepokea maombi pia kutoka kwa vyuo ambavyo bado vina nafasi kuhitaji kuongezwa muda wa udahili.
“Tume imeongeza muda wa udahili kwa kufungua dirisha la udahili kwa awamu ya nne utakaoanza Oktoba mosi hadi 4,mwaka huu,” amesema profesa Kihampa.
Amevitaka vyuo vyote vya elimu ya juu kubainisha proramu zenye nafasi ili kuwawezesha waombaji kufanya maamuzi sahihi wakati wa kutuma maombi ya udahili.
Amewakumbusha waombaji wote kuwa masuala ya yanayohusiana na udahiliama kuthibitisha yawasilishwe moja kwa moja katika vyuo husika na si TCU.
RECOMMENDED FOR YOU:
- CHECK SCHOLARSHIP OPPORTUNITIES TO STUDY ABROAD - CLICK HERE
- HIGH EDUCATION LOAN FOR UNDERGRADUATE AND POST GRADUATE. CLICK HERE
- MAJINA WALIOCHAGULIWA AJIRA ZA SENSA 2022 - Selected Applicants For Census [ DFF ]. Click Here
- 1000+ DAILY GOVERNMENT AND NGOs JOBS VACANCY AVAILABLE TODAY .
- TAARIFA YA HABARI MASAA 24, SUBSCRIBE HAPA YOUTUBE CHANNEL YA Kamatia Online.